EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, June 30, 2013

PICHA ZA MATUKIO YOTE YA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 ZIPITIE HAPA.

MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 APATIKANA NI LUCY CHARLES KUTOKA MWANZA. OMMY DIMPOZ NA MICHAEL ROSS WAKIWASHA MOTO

Babylove Kalalaa akijikusanyia makato!!
Mnataka tena jamani!!!
warembo wote wakaitwa !!

MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 APATIKANA NI LUCY CHARLES KUTOKA MWANZA.

Mrembo Lucy Charles akitabasamu baada ya kuvikwa taji la Redd's miss Kanda ya Ziwa usiku huu.

Kinyanganyiro cha kumtafuta mnyange wa Kanda ya Ziwa kwa mwaka 2013, kimeteguliwa usiku huu kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest baada ya Mrembo Lucy Charles msomi wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino, kuwabwaga warembo wengine 17 waliojitokeza.

Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga akijiandaa kuanza kuita 10 Bora hapa
Top 10.

Tano Bora
Mrembo huyo aliwapagawisha mashabiki wa urembo waliofurika katika ukumbi wa Hotel ya Gold Crest baada ya kujibu swali kwa ustadi lililouliza Ni changamoto ipi kubwa walionayo vijana wa leo.
Mshindi wa pili katika shindano hilo ni Eshe Rashid  na mshindi wa tatu ni Salsha Isdore

Vinara watatu .katikati ni Lucy Charles mshindi wa Redd's miss Lake zone 2013, kulia ni Eshe Rashid kutoka Mara na kushoto ni Salsha Isdore kutoka Geita na wote watatu wanaenda ngazi ya taifa.
Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga

HIVI NDIVYO RAIS KIKWETE ALIVYOWAANDALIA MARAIS SHEREHE FUPI.

 Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mfalme wa Swaziland, King Mswati katika hafla ya chakula cha usiku alichokiandaa kwenye viwanja vya Gymkhana, Dar es Salaam jana usiku, kwa waliohudhuria Mdahalo wa Kimataifa wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Sayansi na Teknolojia kwa Manufaa ya Wote (Global Smart Partinership Dialogue). TBL ni moja kati kampuni zilizofadhli hafla hiyo.
 Mahali palipoandaliwa kwa dina kwenye viwanja vya Gymkhana
 Rais wa zamani wa Msumbiji, Joachim Chisano (kushoto) akikaribishwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernald Membe katika hafla ya chakula cha usiku.
 JK akiwa na Museveni wa Uganda (kushoto), Kingi Mswati wa Swaziland na Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi

Pigo ujio wa Obama •Afuta ziara kwenye mbunga za wanyama za Mikumi, Serengeti

MADHARA ya vurugu za kisiasa mkoani Arusha zinazodaiwa kusababishwa na polisi kukabiliana na wafuasi wa vyama vya upinzani, zimesababisha pigo kubwa kiuchumi katika ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama, Tanzania Daima Jumapili limebaini.
Pigo hilo ambalo limesababisha serikali na mahoteli ya kitalii mkoani humo kukosa mabilioni ya fedha, limetokana na hatua ya rais huyo na ujumbe wake kufuta ziara yake kwenye mbunga za wanyama za Serengeti na Mikumi.

Hatua hiyo imeelezwa kuwa ni pigo kwa serikali ambayo ilitarajia kuingiza mabilioni ya fedha baada ya rais huyo maarufu duniani na ujumbe wake wa watu 700, kuzuru kwenye hifadhi hizo za taifa.
Rais Obama ambaye alianza ziara yake barani Afrika nchini Senegal, alipata fursa ya kutembelea sehemu za utalii na hata alipokuwa nchini Afrika Kusini, alitembelea sehemu ya utalii, hususan gereza alilopata kufungwa Rais wa kwanza mweusi wa nchi hiyo, mzee Nelson Mandela, ambaye kwa sasa yu mahututi.

Habari kutoka ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa zilisema Rais Obama ambaye anatarajiwa kuwasili kesho nchini, akitokea nchini Afrika Kusini, amefuta ziara hizo kwa sababu za kiusalama, hususan hali tete iliyoko mkoani Arusha.

BEYONCE NA VAZI LA KANGA, ILIYOTENGENEZWA NA CHRISTINA MHANDO WA KITANZANIA

clip_image001[6]Christina (katikati)
Utajiskiaje kuona Beyonce akiwa amevaa vazi lililotengenezwa kwa kanga yenye maneno ya Kiswahili? ‘Wawili Ninyi Yawahusu….’ yanasomekana maandishi kwenye vazi alilolivaa mwanamuziki wa Marekani, Beyonce Knowles.clip_image001Vazi hili alilolivaa Beyonce kwenye moja ya show zake za tour ya Mrs Carter, limetengenezwa na mwanamitindo wa Tanzania aishie jijini London Uingereza, Christine Mhando mwenye brand ya Chichia London. Chichia London ndio brand iliyo maarufu sana nchini Uingereza kwa kutengeneza nguo za Kitanzania kwa kutumia Kanga na material mengine Kiafrika.
Hizi ni baadhi ya nguo alizotengeneza.clip_image001[8]
clip_image001[10]clip_image001[12]

SHEMEJI YETU KWA JOKATE HUYU HAPA!

Mwanamitendo maarufu Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ amemwanika mwanaume mpya mtandaoni huku wakiwa wamepozi katika staili ya wapendanao.

Awali, paparazi wetu alitonywa na sosi aliyeomba hifadhi ya jina lake kuwa amemuona mwanaume mpya wa Jokate katika mtandao wa Instagram.

“Nimemuona Jokate na mwanaume wake mpya lakini simjui kwa jina, kama huamini ingia kwenye mtandao wa Instagram uone mtoto wa kike alivyojiachia katika pozi za kimahaba,” alisema sosi huyo.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu aliingia kwenye kilongalonga chake na kuperuzi katika mtandao huo kisha kujionea picha hizo, haraka sana akazisevu katika simu yake.

Aidha, wadau mbalimbali waliopo katika mtandao huo walitoa maoni mbalimbali huku wengi wao wakimpongeza.

Saturday, June 29, 2013

Wema sepetu na Rado ndani ya filamu mpya, ni moto wa kuotea mbali.

Baada ya kufanya vizuri na filamu yake ya maduhu, hatimaye mwigizaji Simon Mwapagata ameanza kutengeneza Filamu yake mpya aliyowashirikisha mastaa mbalimbali akiwemo mrembo kipenzi cha wengi Wema Abraham Sepetu.
 Exclusive: Wema sepetu na Rado ndani ya filamu mpya, ni moto wa kuotea mbali. 2
Akizungumza katika utengenezaji wa Filamu hiyo unaoendelea maeneo mbalimbali ya jijini Dar es salaam, Rado (Simon Mwapagata) amesema kuwa Filamu hiyo itafanyika mjini Dar es Salaam na baadaye mkoani Tanga.

Kitu kipya toka kwa Wolper na Ray - waigiza kama mke na mume.

Vincent Kigosi ama Ray na mrembo Jacqueline Wolper , wapo location wakishoot movie yao mpya ambayo bado hatujaweza kupata jina lake mpaka sasa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu.
 Kitu kipya toka kwa Wolper na Ray - waigiza kama mke na mume. Angalia picha
Katika picha picha hizo walizoziweka kwenye akaunti zao za mtandao mmoja wa kijamii nchini inaonekana wanaigiza kama mke na mume.

“Siye tena kazini new movie, mke wa mtu me hapa nacheza.me en broo ray mwenyezi mungu kua nasi mwanzo hadi tumalize inshaalah ,” ameandika Wolper kwenye moja picha hizo.

Baada ya Wema, Wolper, na Irene Uwoya kuzianika tattoo zao, sasa ni zamu ya Chuchu hans.

Baada ya Wema, Wolper, na Irene Uwoya kuzianika tattoo zao, sasa ni zamu ya Chuchu hans. Ipo kiunoni. Iangalie hapaBaada ya Wema, Wolper, na Irene Uwoya kuzianika tattoo zao, sasa ni zamu ya Chuchu hans. Ipo kiunoni. Iangalie hapa 1Baada ya Wema, Wolper, na Irene Uwoya kuzianika tattoo zao, sasa ni zamu ya Chuchu hans. Ipo kiunoni. Iangalie hapa 2Baada ya Wema, Wolper, na Irene Uwoya kuzianika tattoo zao, sasa ni zamu ya Chuchu hans. Ipo kiunoni. Iangalie hapa 3Baada ya Wema, Wolper, na Irene Uwoya kuzianika tattoo zao, sasa ni zamu ya Chuchu hans. Ipo kiunoni. Iangalie hapa 4Baada ya Wema, Wolper, na Irene Uwoya kuzianika tattoo zao, sasa ni zamu ya Chuchu hans. Ipo kiunoni. Iangalie hapa 5

Baada ya waigizaji kadhaa wa bongo movies kuendelea kuzianika tattoo zao mbalimbali zilizopo kwenye miili yao,sasa ni zamu ya mwigizaji Anyefanya vizuri sana kwenye tasnia ya filamu nchini Chuchu Hans Kichunya kuziweka zake hadaharani baada ya jana kuweka picha kadhaa kwenye mtandao zikionesha tattoo hiyo iliyoko maeneo ya kiunoni kwa juu kidogo.

Huyu anakuwa msanii mwingine tena wa bongo movies kuweka wazi tattoo zake baada ya waigizaji waliozoeleka kwenye jamii kwa tattoo zao kama Wema sepetu, Irene Uwoya, Jacquiline Wolper na Mainda.

Kajala aamua kunyoa kipara; kisa na mkasa? Soma hapa.

Mwigizaji aliyerudi uraiani hivi karibuni Kajala Masanja amefanya mabadiliko makubwa ya mtindo wake wa nywele baada ya kunyoa kipara “kikavu” kichwani mwake.
 Exclusive: Kajala aamua kunyoa kipara; kisa na mkasa? Soma hapa.
Katika picha alizozitoa mwigizaji huyo kupitia kwenye mtandao jana, mwigizaji huyo ameonekana akiwa na kipara tofauti na alivyozoeleka na nywele nyingi siku za nyuma.

Bongomovies.com tuliamua kumtafuta mwanadada huyu ili kujua “kunani”?? na staili hiyo na tulimpigia simu na maongezi yalikuwa kama ifuatavyo:
Bongomovies.com: Mambo kajala, mzima?
Kajala: Mzima, kwema?

Kashfa nzito Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam


HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala, jijini Dar es Salaam imeingia katika kashfa nzito baada ya kuvunja nyumba ya mwanamke mmoja Ashura Swed mkazi wa Upanga kwa maelezo kuwa ipo barabarani.

Katika hali ya kushangaza, manispaa hiyo imemruhusu kujenga eneo hilo hilo mtu mwingine aliyejulikana kwa jina la Bahadur Dewji mwenye asili ya Asia.

Akizungumza na Tanzania Daima, mjukuu wa Ashura, Shamsa Salim ameiomba serikali kuingilia kati sakata hilo ili kuzuia kile alichodai kuwa uonevu wanaofanyiwa na watu wenye uwezo wa pesa.

Akisimulia huku akibubujikwa na machozi, Shamsa alisema Alhamisi ya wiki iliyopita walishangaa kuona nyumba yao namba 897 iliyoko Mtaa wa Mfaume, Upanga ikivunjwa huku wao wakiwa hawana taaarifa yoyote juu ya ubomoaji huo kwa madai kuwa ipo barabarani.

“Ilikuwa Alhamisi, wiki jana, majira ya saa tano asubuhi tulishtuka na kushangaa kuona kundi la watu waliojitambulisha kuwa wafanyakazi wa Manispaa ya Ilala wakivunja nyumba yetu. Tulipowaomba watupatie amri ya mahakama inayowaruhusu kuvunja nyumba yetu hawakutuonyesha badala yake waliendelea kuvunja tu.

Makaburi 250 kuhamishwa Dar


HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam imetangaza kuyahamisha makaburi 250 yaliyopo ndani ya eneo la mradi wa upanuzi wa njia za umeme Kata ya Manzese na Kata ya Ubungo, Mtaa wa Ubungo Kisiwani.

Hatua hiyo ilitangazwa jana na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Mhandisi Mussa Natty katika taarifa yake kwa vyombo vya habari baada ya kupata taarifa ya kuhamisha makaburi hayo kutoka Shirika la Umeme Nchini(TANESCO).

Kutokana na hatua hiyo, amewataka watu wote wenye ndugu au jamaa waliozikwa kwenye eneo hilo kwenda kwenye ofisi za Ofisa Mtendaji wa Kata ya Manzese na Ubungo kujiandikisha wakiwa na barua ya utambulisho kutoka ofisi ya mtaa wanakoishi kabla ya Julai 25.

“Mkurugenzi wa TANESCO anawatangazia ndugu na jamaa za marehemu waliozikwa kwenye makaburi yaliyopo ndani ya eneo la mradi wa upanuzi wa njia za umeme Kata ya Manzese, Mtaa wa Madizini na Kata ya Ubungo Mtaa wa Ubungo Kisiwani, kwamba anakusudia kuhamisha makaburi 250 ili shughuli ya upanuzi wa njia ya umeme iweze kuanza,” alisema Natty katika taarifa yake.

Alisema kwa mujibu wa sheria ya mitaa (Mamlaka za Miji) ya mwaka 1982, kanuni ya mwaka 2008 namba 46(c) Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni itasimamia zoezi hilo kwa kutumia wataalamu wake.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, makaburi hayo yatahamishiwa katika makaburi ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni yaliyopo Tegeta Kata ya Kunduchi baada ya tararibu zote kukamilika.

Hospitali ya Bugando kutibu saratani

SERIKALI imesema Hospitali ya Rufaa Bugando itaanza kutoa tiba ya saratani kwa mionzi hivi karibuni.
Taarifa hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Afrika Mashariki, Dk. Abdulla Juma Saadalla wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Rukia Kassim Ahmed (CUF).
Katika swali lake, mbunge huyo alitaka kujua mpango wa serikali wa kuanzisha kitengo cha wagonjwa wa saratani katika mikoa mingine.

Dk. Saadalla alisema mashine hizo za kutibu kansa kwa mionzi zinatarajiwa kuwasili katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Agosti mwaka huu.
Alisema baada ya mashine hizo kuwasili, wagonjwa wenye matatizo ya saratani kutoka Kanda ya Ziwa wanaohitaji mionzi hawatalazimika kwenda Dar es Salaam kupata huduma hiyo.

Serikali yafuta ushuru wa mafuta.

HATIMAYE serikali imeridhia uamuzi wa wabunge na kukubali kufuta pendekezo la kuongeza ushuru wa bidhaa kwenye mafuta ya dizeli na petroli.

Katika marekebisho hayo, Waziri wa Fedha na Uchumi, William Mgimwa alikuwa amependekeza kuongeza ushuru wa mafuta hayo kwa sh 2 kwenye dizeli na sh 61 kwenye petroli kwa lita.

Kwa mantiki hiyo, alisema kuwa wataendelea kutoza ushuru wa bidhaa wa sh 333 kwa lita katika mafuta ya petroli na sh 215 kwa lita kwenye dizeli.

Wakijadili muswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2013, wabunge walipinga mapendekezo hayo na kuishauri serikali itafute mapato kutoka kwenye vyanzo vipya vilivyoanishwa na Kamati ya Bunge ya Bajeti badala ya kuongeza gharama za maisha kwa wananchi.

Akijibu hoja za wabunge jana kabla ya kupitishwa kwa muswada huo kuwa sheria itakayoanza kutumika Julai mosi mwaka huu, Waziri Mgimwa alisema walikubali ushauri huo ili kuleta unafuu kwa wananchi na kuzuia mfumuko wa bei unaoweza kujitokeza.

Alisema serikali iteendelea kutoza ushuru wa sasa bila kuongeza hata senti, lakini wameongeza ushuru wa mafuta ya taa kufikia sh 425 kwa lita badala ya sh 400.30 zinazotozwa sasa hivi.

BAADA YA KIMWANA HUDDAH KUTINGA CLOUDS FM,DIVA AMIMINA MANENO HAYA HAPA


Kama utakua ni muumini wa twitter lazima utakuwa unajua kinachoendelea kati ya mshiriki wa BBA kutoka Kenya  (2013), Huddah na mtangazaji Diva Loveness love.
kiufupi ni tweef ( bif kupitia twitter) kisa kikiwa ni CMB Prezzo 
Siku ya jana katika interview tuliyofanya na Hudda amesema hana uhusiano na Prezzo, ni rafiki yake tu, na hana beef yoyote na Diva na kwanza hamfaham.
"you know mimi hupenda kutoa maoni yangu, so saa ile mi natoa maoni yangu mtu ana-judge vingine, mi sina bif na Diva, na simjui, na kama uli-notice i only replied three times."
unajua mi niliandika "lol" after seeing her tweet calling Prezzo "baby", why? i just find it funny, so yeye ndio akawa anaandika all that" amesema Hudda
kwa inavyoonekana Diva alikua akisikiliza radio wakati interview ikiendelea, na haikumchukua dakika sifuri, akahusika twitani na kuandika 

ANGA YA RAIS,MMAREKANI HATAKI DHARAU KABISA RAIS OBAMA.



Hii ndiyo hali ya Ulinzi wa Rais Barack Obama White house Marekani

HIVI NDIVYO MREMBO HUDDAH WA KENYA ALIVYOTUA BONGO,ANA BIFU ZITO NA DIVA KISA PENZI LA PREZOO



Huddah akiwaupdate mashabiki wake wa Twitter baada ya kuwasili Dar

Friday, June 28, 2013

JIHADHARI NA UTAPELI ZIARA YA OBAMA

  Habari na Haika Lawere
Jioni hii kuna jamaa kanipigia simu eti yeye ni mtu wa jeshi la police,anahitaji sehemu ya kulaza madereva watakaoendesha msafara wa Obama.
Na akasema Obama anakuja leo sio J3!!Hao madereva wametokea Kenya na Uganda wenye uwezo wa kuzungumza kiingereza,kwa kuwa wa-tz hawajui kuongea kiingereza.Akaniuliza nina vyumba vingapi available nikamuambia 23,vingine 20 viko occupied,akaniambia subiri azungumze na bossi wake,baada ya dk chache akanipigia simu kuwa bossi amekubali hao drivers waje kwetu, tukapigiana mahesabu kwa siku nane watakazokaa kwa bei ya dola 50 per room(aliyosuggest yy)tukapata amount fulani hivi kubwa kidogo!Akasema sasa mama kuna kijana anatoka ofisini anakuletea Cheque sasa hivi ya million 13!!!duh nikashangaa/kufurahi lakini nikashtuka sana how come can this be possible,then kasema 10% yake atakuja kuichukua cheque ikisha clear ila akaniambia ati nimpe uyo kijana anayeleta cheque 500,000 mh??sasa nikamuuliza biashara hatujafanya,sina cash yeyote?cheque ni karatasi tu!!!how come nikupe hela sijaona watu wana check-inn??sina cash??Jamaa asikate simu faster!!!!hahaaaaa hii ilikuwa kali ya kuanzia weekend lol!!!!!Haya service provider wenzangu muwe careful na hii ziara ya Obama isitulize!!!

WEMA SEPETU ASHITAKIWA

MKURUGENZI wa Kampuni ya Filamu ya Endless Fame, Wema Sepetu hivi karibuni amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya majirani zake kumshitaki kwenye serikali ya mtaa kufuatia tabia ya wafanyakazi wake kutiririsha maji machafu mtaani.
 
Wema Sepetu.
Taarifa iliyolifikia blog yetu inadai kuwa, majirani wa Wema katika eneo analoishi, Kijitonyama jijini Dar wamekuwa wakimlalamikia msanii huyo kwa kitendo hicho lakini imeonekana uvumilivu umewashinda.

“Mara kwa mara wafanyakazi wake wamekuwa wakitiririsha maji hapa mtaani sasa leo tumeona tukamshitaki serikali za mitaa ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema mmoja wa majirani wa staa huyo aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.

Juni 26, mwaka huu Ijumaa lilifika kwenye nyumbani kwa Wema na kushuhudia maji yakitoka kisha kuzagaa mtaani na muda mfupi baadaye alifika Afisa Mtendaji wa Kata ya Makumbusho (jina halikufahamika mara moja) ambaye aligonga kwenye nyumba ya Wema, baada ya muda alitoka binti wa kazi aitwaye Bite.

WEMA SASA MAJANGAZZ ATUMIA LUGHA CHAFU KWA WAFANYAKAZI WAKE WA NDANI.

Zaidi Sikiliza video hapo chini 
::Tunawaomba radhi kutikana na lugha chafu iliyokuwepo kwenye video clip hii::

MICHELLE OBAMA POSTS FIRST INSTAGRAM POSING WITH SENEGALESE STUDENTS.

First Lady Michelle Obama christened her new Instagram account posing with students from Martin Luther King Middle School in Dakar, Senegal.

"You all are role models for my daughters, which is why I brought them here today - so that they could be inspired by you just like I am," she wrote in a caption.

President Barack Obama, first lady Michelle and their daughters Malia and Sasha kicked off their trip to Africa Wednesday in a flurry of social media, hoping to attract and engage young Americans.

MIZENGO PINDA ATAKIWA KUWAOMBA MSAMAHA WATANZANIA

Akizungumza na waandishi wa habari jana Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo-Bisimba amesema kitendo cha Waziri Mkuu Bizengo Pinda kuruhusu matumizi ya nguvu kwa polisi dhidi ya raia ni cha kulaaniwa na wapenda haki wote na amemtaka waziri mkuu kuwaomba radhi watanzania.  
KUPINGA KAULI YA WAZIRI MKUU "Wapigwe tu" ALIYOITOA BUNGENI TAREHE 20/06/2013

Taarifa hii ni matokeo ya ufuatiliaji wa utendaji wa shughuli za Serikali kama zinavyowasilishwa bungeni na kauli ya Waziri Mkuu (Mtendaji Mkuu wa shughuli za serikali Bungeni) aliyoitoa, Alhamisi ya tarehe 20 Juni 2013, wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo. 

Waziri Mkuu Pinda, alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama, hususan Jeshi la Polisi kuwapiga wananchi watakao kaidi na kupinga amri halali ya jeshi hilo. Katika tamko hilo, Pinda alisema Serikali imechoshwa na vurugu na kwamba hakuna namna nyingine ya kupambana na wananchi wanaodharau vyombo vya dola zaidi ya kipigo. 

Waziri Mkuu Pinda alitoa msimamo huo Bungeni, wakati akijibu swali la Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM), aliyetaka kujua hatua zinazochukuliwa na Serikali kufuatia kuwa na matukio ya vurugu ya mara kwa mara nchini, hususan huko Mtwara na Arusha.

Picha za siku na Linah na Agness Masogange.


BIBI YAKE OBAMA MAMA SARAH OBAMA KUJA TANZANIA KUMSALIMIA MJUKUU WAKE ATAKAPOWASILI DARESALAM.

SIKU CHACHE KABLA YA ZIARA YA RAIS WA MAREKANI KUJA NCHINI TANZANIA IMEFAHAMIKA KUWA BIBI YAKE NA RAIS OBAMA MAMA SARAH OBAMA ANATARAJIA KUJA NCHINI TANZANIA KUJA KUMSALIMIA MJUKUU WAKE HUYO.

HISPANIA imeitoa Italia katika Kombe la Mabara-Fainali ni Brazil vs Hispania.

HISPANIA imeitoa Italia katika Kombe la Mabara kwa ushindi wa matuta wa 7-6 mjini Fortaleza, kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120 katika mchezo wa Nusu Fainali
 
Kikosi cha Hispania kilikuwa: Casillas, Arbeloa, Sergio Ramos, Pique, Jordi Alba, Xavi, Busquets, Iniesta, Pedro/Mata dk79, Torres/Javi Martinez dk94 na Silva/Jesus Navas dk52.
 
Italia: Buffon, Maggio, Bonucci, Barzagli/Montolivo dk45,Chiellini, Candreva, De Rossi, Pirlo, Marchisio/Aquilani dk79, Giaccherini na Gilardino/Giovinco dk91.
Off target: Italy blinked first in the shout-out when Leonardo Bonucci fired over at 6-6
Anakosaaa: Leonardo Bonucci mkwaju wake uliota mbawa
Decisive: Jesus Navas stepped up to score the winning penalty and send Spain to the final
Ya ushindi: Jesus Navas alifunga ya mwisho, chini anashangilia
Jesus Navas
Jesus Navas
Glamour: Worldwide superstar Shakira was in the stands in Fortaleza
Shakira alikuwapo jukwaani Fortaleza 

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate