EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, August 31, 2012

WA5 WATINGA FAINALI YA SHINDANO LA REDD'S MISS KANDA YA MASHARIKI TALENT, KUUMANA KESHO MORO


 Warembo wa 5, waliofanikiwa kutinga katika hatua ya Fainali ya shindano la Miss Kanda ya Mashariki, baada ya kuchuana vikali katika shindano lao dogo la Redd's Miss Kanda ya Mashariki Talent, lililofanyika jana usiku kwenye Hoteli ya Usambara, mjini Morogoro. Kutoka (kushoto) ni Mrembo, Joyce Baluhi, Shakhila Hassan, Zuhura Gola, Irene Veda na Salvina Kibona, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi.
 Mrembo, Rose Lucas, akionyesha umahiri wake kwa kushambulia jukwaa ipasavyo kujaribu bahati yake kwa kuwakomvis Majaji, wakati wa shindano hilo.
 Mrembo, Shakhila Hassan, akiimba wimbo wa dini, Ebeneza na kuwapagawisha Majaji na mashabiki waliohudhuria onyesho la mpambano huo jana usiku.
 Mrembo, Joyce Baluhi, akisebeneka na wimbo wa Demu Mwigizaji wa Tunda Man, na kuwakosha vilivyo, Majaji na mashabiki waliohudhuria shindano hilo.
 Mrembo, Irene Thomas, akishambulia jukwaa kwa kucheza Dancehall........
 Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kushoto) akiwa meza kuu na Miss Tanzania 2010, Geneviv Emmanuel (kulia) na Miss Morogoro 2010, Asha Saleh, wakifuatilia shindano hilo.
 Baadhi ya wadhamini wa shindano hilo, pia walikuwepo kuwakilisha, (kushoto) ni mmoja kati ya wadhamini wa shindano hilo, Kitwe General Traders, ambapo pia wadhamini  Kampuni ya SPM:- Sufiani Photo Magic, Redd'd, Dodoma Wine, Usambara Safari Lodge, Chilakale Resort, B-Ze Hotel, Clouds Fm, Endepa, Gazeti la Jambo Leo na Simple & Easy Car.
              Sehemu ya mashabiki waliohudhuria shindano hilo.
 Sehemu ya mashabiki waliohudhuria shindano hilo, 'kuona na kunywa kikali'.....
 Washiriki wakicheza wimbo wao wa ufunguzi wa shoo hiyo kwa pamoja.
 Majaji wakishauliana jambo wakati shindano hilo likiendelea..........
 Hapa ni mshiriki, Irene Veda, akijifua kwa kupuliza Sax phone kabla ya kuanza kwa shindano hilo...
 Hapa ni kabla ya kuanza shindano hilo, warembo wakipiga picha ya pamoja kushoo Love.
                                 Namba za Bahati zilizotinga Tano Bora
                  Mrembo, Irene Veda, akiimba na kupuliza Sax Phone......

TAMKO LA TGNP KULAANI KAULI ZA DC WA KOROGWE

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
DC Korogwe awajibishwe kwa udhalilishaji

Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), tumesikitishwa sana na kauli iliyotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga Ndugu Mrisho Gambo, kwa  mwanasheria wa Halmashauri hiyo Bi. Najum Tekka, kuhusu uhalali wa shahada aliyonayo hususan kuihusisha shahada hiyo na vitendo vya ngono! Kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari ikiwepo gazeti la Majira Augosti 29,2012 Uk.3

Kauli hii ni udhalilishaji na ukiukwaji mkubwa wa haki za wanawake na inaenda kinyume na misingi ya kuzingatia usawa sanjari na Katiba ya nchi ; Uwezeshaji wa wanawake na utekelezaji wa Maazimio ya Haki na  Usawa katika ngazi za Kimataifa Kikanda na Nchini Tanzania.

Aidha kauli hii, inalenga kupotosha na kukatisha tamaa juhudi kubwa wanazofanya wanawake na wasichana katika  kupata elimu na mafanikio mbalimbali nchini Tanzania. Zaidi ya hapo, kauli hii inadhalilisha na kushusha hadhi ya vyuo vya elimu ya juu vinavyofanya kazi kubwa ya kutoa elimu kwa Watanzania.

Kutokana na kauli hiyo  DC  amekiuka maadili ya uongozi wa umma na kukidhalilisha kiti cha ukuu wa wilaya na kiongozi Mkuu wa nchi aliyemteua kushika wadhifa huo. Aidha kauli ya kiongozi huyo ya kutimia  mahakama kutetea hoja yake , kunaashiria ubabe , ujeuri, vitisho, kiburi na dharau  ya  kutaka kuingilia uhuru wa mahakama na ajenda binafsi isiyokuwa na maslahi kwa wanawake na umma wa Watanzania

Kutokana na kauli hiyo ya udhalilishwaji ,sisi  wanaharakati  wa ukombozi wa wanawake Kimapinduzi, usawa wa kijinsia, haki za kibinadamu demokrasia tunalaani vikali kauli za DC na kutoa  Rai ifuatayo:

1.      Mkuu wa Wilaya  Ndugu Mrisho: amwombe radhi Mwanasheria Bi.  Najum Tekka, kwa kosa la  kumdhalilisha kijinsia

2.      Tume ya maadili ya utumishi wa umma, na Mamlaka nyingine za kinidhamu zimchukulie hatua za kinidhamu Ndugu Gambo kwa kutumia lugha ya kudhalilisha watumishi kinyume na maadili.

3.      Wanawake  wote, wanaume, vijana wa kike na kiume kuendelea na mapambano dhidi ya  mfumo dume na mifumo yote kandamizi, kushikamana katika kudai misingi ya kisheria,  uwajibikaji  inayozingatia usawa na haki na kukataa kudhalilishwa katika ngazi binasfi na za umma !.

Imetolewa  Dar es salaam leo 31/08/2012 na:
Usu Mallya
Mkrugenzi Mtendaji TGNP

IJUMAA SEXIEST GIRL 2011/2012: JACK WOLPER ‘OUT’, WEMA AGNES NI KIZAAZAA


 

HUKU wadau wakiwa na shauku kubwa ya kumjua mshindi wa shindano hili la kumsaka staa wa kike mwenye mvuto ambaye hajaolewa 

‘The Ijumaa Sexiest Girl’, hatimaye kura za wasomaji zimeamua msanii wa filamu, Jackline Wolper kutoa mkono wa kwaheri.Mratibu wa shindano hili, Imelda Mtema alisema: 


“Mtifuano ulikuwa mkali sana na hii ilitokana na ukweli kwamba, wote waliobaki ni wakali kuanzia sura hadi maumbo yao.

 Wopler ametolewa na sasa kimbembe ni kati ya Wema na Agnes.”
 

 Kufuatia matokeo hayo ya Wolper kuchapa lapa, sasa wanabaki Wema na Agnes ambao watapigiwa kura kwa wiki mbili kabla ya kumpata mshindi. 


Ili kushiriki katika hatua hii muhimu ya kumpata mshindi, andika jina la mshiriki kisha litume kwenda namba 0786-799120.

GADNER G. HABASH AHAMIA RADIO TIMES 100.5 FM, KURINDIMA NA KIPINDI KIPYA CHA “MASKANI”

Kapten Gadner Habash ambaye amejiunga na kituo hicho cha redio na kutangazia umma rasmi akizungumza na wanahabari pamoja na watangazaji wenzake, wanaofuatia katika picha ni Scholastica Mazula, Criford Ndimbo na Dida wa Mchops.
 Mtangazaji wa Radio Times 100.5 Scholastica Mazula akizungumza na waandishi wa habari kwenye magahawa wa City Sports Lounge Posta jijini Dar es salaam wakato alipomtambulisha rasmi Kapten Gadner Habash ambaye amejiunga na kituo hicho cha redio hiyo. Hivi karibuni atakuja na kipindi kipya kinachokewanda kwa jina la “Maskani” kitakachozungumzia mambo mbalimbali katika jamii, katika picha kushoto ni Gadner G. Habash mwenyewe na kulia ni Mtangazaji wa kipindi cha michezo Cliford Ndimbo.
 Baadhi ya watayarishaji wa vipindi na watangazaji katika redio hiyo watatu kutoka kulia ni mkoloni aliyewahi kuvuma na kundi la Wagosi wa Kaya.
Kapten Gadner Habash kushoto akipozi kwa picha wa mastaafu wenzake wapya kutoka kulia ni Dida wa Mchops, Natasha na Scholastica Mazula.
                                                 CHANZO: http://www.hakingowi.com

LEO NI LEO MISS MWANZA 2012

Warembo Redds Miss Mwanza 2012/13 wakiwa katika pozi.
Na Mwandishi Wetu
FAINALI za Miss Mwanza 2012, zinatarajiwa kuchukua nafasi leo ndani ya Ukumbi wa Yacht Club.
Akizungumza na Ijumaa, mratibu wa mtanange huo, Peter Omar alisema: “Kila kitu kipo sawa, maandalizi ni mazuri, tunachosubiri ni huo muda ufike ili tuweze kumpata mshindi.”
 
Kwa upande wa burudani Peter alisema, wakongwe wa taarab nchini, Malkia Khadija Kopa na gwiji Mwanahawa Ali, wanatarajiwa kuoneshana umwamba stejini sambamba na burudani nyingine kibao.
“Miss Mwanza ya mwaka huu ni funga kazi. Watakaokuja Yacht Club leo, watashuhudia shoo kali ambayo haijawahi kutokea. Kwanza tuna warembo wazuri, hii ina maana Miss Tanzania 2012, atatokea Mwanza,” alijigamba Peter.

MADAMU RITA AOMBWA UCHUMBA NA ‘SERENGETI BOY’


Rita Paulsen ‘Madam Rita’.
CHIEF Judge wa Shindano la Epiq Bongo Star Search, Rita Paulsen ‘Madam Rita’ hivi karibuni amejikuta akiombwa uchumba na vivulana nyenye umri mdogo ‘serengeti boys’ kupitia ukurasa wake wa Facebook.
Akipiga stori na Ijumaa, Madam Rita alisema kuwa, alianzisha ukurasa huo kwa ajili ya kubadilishana mawazo na watu mbalimbali lakini akashangazwa na baadhi ya wavulana ambao wamempenda kiasi cha kufikia hatua ya kumuomba uchumba.
 
“Huwezi amini sina siku nyingi sana tangu nimeanzisha ukurasa huu lakini nina marafiki wengi na wapo ambao wanaomba kuwa marafiki wangu, huko nimeshapata wachumba sita tena wengine wakiwa na umri mdogo sana,” alisema Madam Rita na kuongeza:
“Kimsingi nawaheshimu watu wa rika zote kutoka mikoa yote kwani wao ndiyo wadau wakubwa wa EBSS na wameifanya program hii kujipatia umaarufu mkubwa na kufika hapa ilipo sasa.”

Jopo la Majaji watatu kusikiliza Rufaa ya umri wa Elizabeth Michael "Lulu" Septemba 17

MAHAKAMA ya Rufani imepanga kusikiliza shauri la umri wa msanii wa filamu Elizabeth Michael, maarufu kama Lulu, Septemba 17 mwaka huu mbele ya jopo la majaji watatu wa mahakama hiyo ambao ni Jaji Bernard Luanda, Jaji January Msoffe na Jaji Katherine Oriyo.

Rufaa hiyo ni ile iliyowasilishwa na mawakili wa upande wa mashitaka wakiomba kupitiwa uamuzi wa Mahakama Kuu uliotolewa na Jaji Dkt. Fauz Twaibu ambao alikubali maombi ya Lulu kusikiliza maombi ya utata wa umri wake.

Siku ambayo Mahakama Kuu ilitarajia kuanza kusikiliza maombi ya uchunguzi wa umri wa Lulu, upande wa mashtaka ulidai kuwa umewasilisha Mahakama ya Rufani maombi ya marejeo ya uamuzi huo, jambo ambalo lilifanya Mahakama Kuu iahirishe uchunguzi huo kusubiri uamuzi wa Mahakama ya Rufani.

Breaking News,Ak Classic Cosmetics is officially Beauty Partner of Miss Universe 2012...

Pozi kwa pozi na Mamodoz!!

The super modoz wakiwa ktk pozi ndani ya AK classic

Ajajajajajajajah!!

From left, Rose,Winfrida,Seif &Seif(miss Universe coordinator) & AK classic!

Put the swag on....

Miss Universe(Winfrida Dominic) akikabidhiwa Zawadi zake na AK!
Via akclassic.blogspot.com
Katuwakilishe Vyema dada!!!
AK akimtayarishia miss Universe(Winfrida) madiko diko ya urembo!!
Wanapatikana>>>>>>>>>>> MADUKA YAPO KINONDONI MANYANYA na SINZA KUMEKUCHA
Busy selecting what is best 4 for her complexion!!

Aya mama chagua ukatuwakilishe vizuri uko Poland.

Mambo yakaanza sasa,moja baada ya moja...

Eye shadow nayo twendeeeeeeeeeeee
Via akclassic.blogspot.com

  

Majina ya Kata zitakazofanya uchaguzi mdogo wa Madiwani, Oktoba 2012

Tume ya Taifa ya Uchaguzi  (NEC), imetja majina ya Kata zitakazofanya uchaguzi mdogo wa Madiwani kutokana na wagombea walioshinda katika uchaguzi wa Madiwani uliofanyika Oktoba 31, 2010  baadhi yao kufariki, kupoteza sifa na kujiuzulu.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa tume hiyo, Jullius Mallaba, alisema maandalizi yamekamilika na upigaji kura utafanyika katika vituo vilivyotumika wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Aidha, Mallaba alisema watakaohusika katika upigaji kura ni wale walioandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura ambapo wapiga kura wanatakiwa kwenda kwenye vituo vya kupigia kura wakiwa na kadi zao.

Mallaba alizitaja kata hizo ambazo uchaguzi utafanyika ni:
  • Arusha - Bangata 
  • Arusha - Daraja Mbili
  • Dodoma - Msalato
  • Dodoma - Mpwapwa 
  • Pwani/Bagamoyo - Magomeni
  • Geita - Lwezera 
  • Shinyanga - Bugarama
  • Shinyanga - Mwananza
  • Tanga/Korogwe - Vugiri 
  • Tanga/Korogwe - Tamota 
  • Lindi/Liwale - Makata 
  • Lindi/Nachigwea - Mnero
  • Njombe/Ludewa - Mlangali
  • Njombe/Makete - Luwumbu
  • Ruvuma/Mbinga - Mpepai 
  • Ruvuma/Songea - Mletele
  • Tabora/Sikonge - Ipole
  • Tabora - Miyenze 
  • Tabora - Karitu
  • Mbeya/Mbozi - Mpapa
  • Mwanza/Misungwi - Lubili
  • Kilimanjaro - Kilema Kusini
  • Kilimanjaro - Nanjara
  • Kilimanjaro - Neha 
  • Morogoro/Mvomero - Mtibwa 
  • Morogoro/Ulanga - Mahenge
  • Mtwara/Nanyumbu - Likokona
  • Mtwara/Newala - Kitangiri

Mahakama yawaachia huru Wanachuo 51 wa UDSM

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imewaachia huru wanafunzi 51 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) waliokuwa wakikabiliwa kwa pamoja na mashitaka ya kufanya mkusanyiko usio halali tarehe Novemba 11 mwaka 2011, eneo la Mlimani la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kusababisha uvunjifu wa amani eneo la chuo hicho.

Wanafunzi hao waliachiwa jana na Hakimu Walialwande Lema aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo baada ya upande wa mashitaka ulioongozwa na Wakili wa Serikali, Ladslaus  Komanya kushindwa kuleta mashahidi mahakamani huku wakitoa sababu mbalimbali. Komanya alidai kuwa  washtakiwa hao wakiwa kwenye mkusanyiko huo haramu kwa lengo la kufanya mgomo, askari wa Jeshi la Polisi waliwataka watawanyike, lakini hata hivyo wanafunzi hao walikaidi amri hiyo na kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.

Hata hivyo washitakiwa hao ambao walifikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa jeshi la polisi, walikana mashtaka hayo na waliachiwa huru baada ya kukamilisha masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja wa kuaminika ambaye alisaini bondi ya Shilingi milioni moja.

Baada ya kuachwa huru, wanafunzi hao waliondoka mahakamani hapo kwa furaha huku wakikumbatiana na wengine wakisali.

Akitoa uamuzi huo jana, Hakimu Lema alisema kuwa anatupilia mbali maombi ya upande wa mashitaka yaliyokuwa yakiomba ahirisho la kesi hiyo kwa mara nyingine wakidai kuwa mashahidi wao ambao ni askari wako katika Sensa ya Watu na Makazi.

Lema alisema kuwa sensa ni muhimu kama ilivyo kesi hiyo, lakini maombi yao hayakufuata taratibu za sheria ambapo kwa mujibu wa kifungu cha sheria cha 225 (4) Sheria ya  Mwenendo wa Mashauri ya Jinai (CPA), sura ya 20 kwa sababu upande wa mashtaka ulishindwa kuliendesha shtaka hilo.

“Agosti 13 mwaka huu kulikuwa na ahirisho ambapo sababu ilikuwa hakuna mashahidi kwa sababu wako katika mgomo wa madaktari, leo tena mnaleta sababu kuwa wako katika sensa inaonesha mmedharau amri ya Mahakama,” alisema Hakimu.

Alisema amri ya mwisho aliyoitoa ilikuwa ahirisho la Agosti 13 mwaka huu hivyo upande wa mashitaka umedharau amri ya Mahakama na kwa maana hiyo anawaachia huru washitakiwa wote chini ya kifungu cha sheria ya Mwenendo wa makosa ya jinai kifungu cha 225 (5) sura ya 20.

Awali wakili wa upande wa mashitaka, Prosper Mwangamila alidai kuwa kesi ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa akaomba iahirishwe hadi Jumatatu. Wakili wa washitakiwa hao, Reginard Martin akijibu hoja hiyo aliiomba Mahakama kutokubali ombi hilo na badala yake kesi ifutwe washitakiwa waachiwe huru.

Baadhi ya majina ya wanafunzi walioachwa huru ni Mwambapa Elias, Evarist Ambrose, Baraka Monas, Hellen Moshi, Alphonce Lusako, Matrona Babu, Rolanda Wilfred, Godfrey Deogratius, Moris Denis and Evon Gumbi.Others are Lugiko Mathias, Ndimbo Jabir, Evarist Wilson, Cornel Rwaga Mushi, Mlazi Kumbuka, Rehema Munuo, Glory Masawe, Happy Amulike, Elias Mpangala, Frida Timothy, Stella Mofe, Betwel Martin, Mmasi Stephen na Lugemalila Venance na wengineo.
 
Taarifa via HabariLeo na Mwananchi

Wateja wa Precision Air kukata tiketi za usafiri kupitia huduma ya M-Pesa.


Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara cha kampuni ya Precision Air, Patrick Ndekana(kushoto)akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mkataba na Vodacom Tanzania ambapo wateja wataweza kulipia tiketi za usafiri kupitia huduma ya M-Pesa,kulia ni Mkuu wa kitengo cha huduma za fedha wa Vodacom Tanzania Bw. Innocent Ephraim.
*******
Kampuni ya usafiri wa anga ya Precision air hii leo imeingia kwenye mkataba na Vodacom Tanzania ambapo wateja wataweza kulipia tiketi za usafiri kupitia huduma ya M-Pesa.

Ili kufanya malipo mteja atatakiwa kupiga namba *150*00# na kuchagua malipo ya bili kupitia orodha ya M-pesa na kuingiza namba ya biashara ya Precision Air ambayo ni 333777  ikifuatiwa na namba ya malipo na kiasi cha fedha itakayolipwa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huo, Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara cha kampuni ya Precision Air, Patrick Ndekana, amesema kuwa njia hiyo ni ya haraka, rahisi na itaokoa muda kwa wateja.

“Tunafurahi kuingia katika ushirikiano huu na Vodacom Tanzania, Tunawahimiza wateja wetu kutumia huduma hii ili kuokoa muda na kufanya malipo yao katika njia ambayo ni rahisi na ya haraka,” alisema Ndekana.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Kifedha cha Vodacom Tanzania, Innocent Ephraim, alibainisha kuwa ushirikiano huo utatoa njia badala katika malipo ya tiketi, na kusisitiza kuwa huduma ya M- pesa ni salama, haraka na niya uhakika, kwa kuwa imeleta mapinduzi katika huduma mbalimbali za kifedha tangu kuanzishwa kwake miaka mimne iliyopita.

“Tunaamini kuwa tutatoa huduma bora kwa wateja wetu. Tunajivunia ushirikiano huu na tunatarajia utakuwa na mafanikio makubwa katika kukidhi mahitaji ya huduma kwa wateja wetu,” alisema Ephraim.

Huduma ya M-Pesa ya Vodacom Tanzania ina mawakala zaidi ya elfu 20,000 nchini kote, na ni pekee ambayo inaongoza, kwa usalama na ubora katika kukidhi mahitaji ya huduma za kifedha kwa Watatanzania walio wengi.

Kampuni ya Precision Air inatoa huduma zake katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, na kufika katika maeneo mengi ya nchi kwa siku.

Sasa kampuni hiyo ina ndege tano zenye uwezo wa kubeba abiria sabini aina ya ATR 72-500, na ATR 42 yenye uwezo wa kubeba abiria arobaini na nane na ndege nyingine tatu aina ya Boeng 737. Na sasa iko katika mpango wa kuongeza ndege nyingine aina ya E- jets na ATR.
Mkuu wa kitengo cha huduma za fedha wa Vodacom Tanzania Bw. Innocent Ephraim,akionesha bango lenye maelekezo muhimu ya kufuatwa ambayo yatawafanya wateja wapate huduma ya kulipia tiketi za usafiri kupitia huduma ya M-Pesa kwa urahisi zaidi,kushoto ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara cha Precision Air, Patrick Ndekana.
Baadhi ya wafanyakazi wa Precision Air wakifatilia kiumakini mkutano wa waandishi wa habari kuhusiana na mkataba wa Vodacom Tanzania na kampuni yao ambapo wateja wa Precision Air wataweza kulipia tiketi za usafiri kupitia huduma ya M-Pesa.
Waandishi wa habari wakiwa kazini wakati wa Precision Air na Vodacom Tanzania walipokuwa wakitangaza mkataba kuhusiana na wateja wa Precision Air kuweza kulipia tiketi za usafiri kupitia huduma ya M-Pesa.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO KIFO CHA ASKOFU KIKOTI

Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akitoka kwenye jengo la kiaskofu la Jimbo la Mpanda mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo ya kifu cha Askofu wa Jimbo la Mpanda Pascal Kikoti kilichotokea juzi katika Hospotari ya Rufaa ya Bugando Mwanza.
Askofu wa Jimbo la Sumbawanga Damiano Kiarusi akiwa na Makamu wa Askofu wa Jimbo la Mpanda Padri Patrick Kasomo mara baaa ya kuagana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipo kuwa amekwenda kusaini kitabu cha maombolezo cha kifo cha Askofu Pascal Kikoti.

Kaburi likiwa limeandaliwa tayari kwa ajiri ya mazishi ya Askofu wa Jimbo la Mpanda Pascal Kikoti aliyefariki hapo juzi huko Hospitari ya Bugando mwanza atazikwa siku ya Juma mosi katika Kanisa la Kiaskofu la Parokia Kuu ya Mpanda.

MAMA HAWA NGULUME AFARIKI DUNIA.

Bi Hawa Ngulume enzi za uhai wake.
Bi Hawa Ngulume, aliyewahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Bagamoyo na Mbarali, amefariki dunia jijini Dar es Salaam jana asubuhi. Mama Ngulume ambae pia ni mama mwenye nyumba wangu amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kansa kwa kipindi kirefu na mauti yamemfika akiwa katika hospitali ya Lugalo jijini Dar. 
 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana taratibu za mazishi zinaandaliwa na taarifa kamili itatolewa hapo baadaye.Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AMINA

BREAKING NEWS: CRISTIANO RONALDO ANARUDI MANCHESTER..... KUFANYA NINI?

Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno na Real Madrid Cristiano Ronaldo atarudi kwa mara nyingine kwenye jiji la Manchester baada ya kuondoka takribani miaka mitatu iliyopita.

Ronaldo ambaye alikaa kwenye jiji la Manchester kwa misimu mitano akiwa anaichezea klabu ya Manchester United kabla ya kuuzwa kwenda Real Madrid, atarudi kwenye jiji hilo kwa ajili ya kucheza mechi ya Champions league dhidi ya Mabingwa wa England Manchester City. Madrid wamepangwa kundi D, wakiwa  na City, Ajax, na Dortmund.

Haya ndio makundi yote ya Champions league msimu wa 2012-13


Group A

Team Pld W D L GF GA GD Pts
Portugal Porto 0 0 0 0 0 0 0 0
Ukraine Dynamo Kyiv 0 0 0 0 0 0 0 0
France Paris Saint-Germain 0 0 0 0 0 0 0 0
Croatia Dinamo Zagreb 0 0 0 0 0 0 0 0

Group B

Team Pld W D L GF GA GD Pts
England Arsenal 0 0 0 0 0 0 0 0
Germany Schalke 04 0 0 0 0 0 0 0 0
Greece Olympiacos 0 0 0 0 0 0 0 0
France Montpellier 0 0 0 0 0 0 0 0

Group C

Team Pld W D L GF GA GD Pts
Italy Milan 0 0 0 0 0 0 0 0
Russia Zenit St. Petersburg 0 0 0 0 0 0 0 0
Belgium Anderlecht 0 0 0 0 0 0 0 0
Spain Málaga 0 0 0 0 0 0 0 0

Group D

Team Pld W D L GF GA GD Pts
Spain Real Madrid 0 0 0 0 0 0 0 0
England Manchester City 0 0 0 0 0 0 0 0
Netherlands Ajax 0 0 0 0 0 0 0 0
Germany Borussia Dortmund 0 0 0 0 0 0 0 0

Group E

Team Pld W D L GF GA GD Pts
England Chelsea 0 0 0 0 0 0 0 0
Ukraine Shakhtar Donetsk 0 0 0 0 0 0 0 0
Italy Juventus 0 0 0 0 0 0 0 0
Denmark Nordsjælland 0 0 0 0 0 0 0 0

Group F

Team Pld W D L GF GA GD Pts
Germany Bayern Munich 0 0 0 0 0 0 0 0
Spain Valencia 0 0 0 0 0 0 0 0
France Lille 0 0 0 0 0 0 0 0
Belarus BATE Borisov 0 0 0 0 0 0 0 0

Group G

Team Pld W D L GF GA GD Pts
Spain Barcelona 0 0 0 0 0 0 0 0
Portugal Benfica 0 0 0 0 0 0 0 0
Russia Spartak Moscow 0 0 0 0 0 0 0 0
Scotland Celtic 0 0 0 0 0 0 0 0

Group H

Team Pld W D L GF GA GD Pts
England Manchester United 0 0 0 0 0 0 0 0
Portugal Braga 0 0 0 0 0 0 0 0
Turkey Galatasaray 0 0 0 0 0 0 0 0
Romania CFR Cluj 0 0 0 0 0 0 0 0

Via shaffihdauda

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate